Tarehe 5 Juni,2012, mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ambaye amelemaa baada ya kupata ajali ya gari, Bwana Athumani Hamisi (pichani), aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Maelezo, Dar es Salaam, na kutoa taarifa iliyojenga taswira kuwa ametelekezwa na TSN pamoja na Serikali.

TSN inapenda kufafanua kuwa Serikali na kampuni hii, ambayo ilimwajiri Athumani tarehe 1/09/2006 kama Mpiga picha Mwandamizi, wamemhudumia mfanyakazi huyo kikamilifu tangu alipopata ajali tarehe 12 Septemba, 2008 hadi sasa, na huduma hiyo inaendelea.

Baada ya kutokea ajali hiyo, TSN kama mwajiri ilisimamia matibabu yake ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI) mpaka Serikali, kwa kupitia Wizara ya Afya ilipomhamishia  Netcare Rehabilitation Hospital nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

Serikali ililipia gharama za matibabu yake yote akiwa Afrika Kusini kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, ambayo yanazidi shilingi milioni mia moja. Gharama hizo ni pamoja na ununuzi wa kigari maalum ambacho Athumani anatumia sasa.

TSN kama mwajiri ililipa nauli ya ndege kwenda na kurudi pamoja na posho ya kujikimu ya mgonjwa pamoja na ndugu wasindikizaji ambao ni Bw. Hassan Hussein  na  Bi. Mirriam Malaquias.Posho ya kujikimu ilikuwa USD 6,210 sawa na Shilingi 9,315,000, na  nauli kwa watu watatu ilikuwa ni Shilingi 3,535,869.92. Athumani aliendelea kupatiwa huduma akiwa huko Afrika Kusini kwa gharama za Serikali na TSN mpaka aliporejea nchini tarehe 08/05/2010. Gharama zilizolipwa na kampuni kwa mfanyakazi huyu hadi sasa ni takriban shilingi million 52.

Athumani aliporejea nchini alilakiwa na wafanyakazi na viongozi wa TSN na kupangiwa chumba hoteli ya Holiday Inn wakati utaratibu wa kumtafutia nyumba ya kupanga ukikamilishwa. Kampuni ilitumia kiasi cha Shilingi 1,756,979.50 kulipia hoteli. Baadaye alipelekwa kwenye nyumba ambayo alipangiwa na Kampuni katika eneo la Sinza Vatican ambapo ndipo bado anaishi hadi hivi sasa. Gharama ya nyumba kwa mwaka wa kwanza 2010 ilikuwa ni Shilingi 4,200,000 au Shilingi 350,000 kwa mwezi.  Mwaka 201 mwenye nyumba alipandisha kodi hadi 400,000 kwa mwezi ambapo Kampuni ililipia Shilingi 4,800,000. Kodi hiyo imeishia Mei mwaka huu na kampuni imeshafanya mazungumzo na mwenye nyumba ili Athumani aendelee kuishi hapo kwa muda wakati mipango endelevu ya ustawi wake inafanywa kwa kuzingatia taratibu za ajira.

Mnamo tarehe 8/12/2010 Athumani alirudi tena Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake na matibabu yaligharimiwa na Serikali wakati TSN iligharamia nauli yake na ya muuguzi wake, pamoja na posho ya kujikimu Shilingi 6,300,000/-.


Pamoja na bwana Athumumai kulala kitandani kwa muda wote huo ameendelea kulipwa mshahara kamili bila kukatwa kama mfanyakazi wa kawaida ikiwa ni msaada wa kampuni kwa kuzingatia ulemavu alioupata.Mshahara aliolipwa kwa muda wote aliokuwa anaugua ni kiasi cha shilingi 26,773,000. Vile vile kampuni ilimlipa muuguzi toka Afrika Kusini ambaye alikuwa anamhudumiaa Athumani  Rand 12,500 kama mshahara wake.

Kuanzia Januari 2011, mshahara wa Athumani umejumuisha asilimia 15 kama posho ya nyumba ambayo wafanyakazi wote wanalipwa. Aidha  Athumani yupo kwenye mpango wa bima ya afya anayolipiwa na kampuni, ambayo inamwezesha yeye na familia yake kuweza kutibiwa katika hospitali yoyote hapa Tanzania.  Kampuni inamlipia Shilingi 68,449.20 kila mwezi na bima hiyo ndiyo inayogharamia matibabu yake yote hapa nchini.

Bwana Athumani anapatiwa usafiri na TSN mara mbili kwa wiki kumtoa nyumbani hadi Muhimbili na kurudi kwa ajili ya mazoezi ya viungo.  

Imetolewa na
OFISI YA MHARIRI MTENDAJI
08.6.2012





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Watu waanze kukata bima sasa sio kutegemea huruma ya mwajiri, huyu mwandishi ashukuru Mungu yuko serikalini angekuwa sekta binafsi mhh!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Watu waanze kukata bima sasa sio kutegemea huruma ya mwajiri, huyu mwandishi ashukuru Mungu yuko serikalini angekuwa sekta binafsi mhh!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Kwa kifupi hapo TSN mnasafisha mikono kwa kutupa gharama za mwajiri wenu adharani,nafikiri mnakiuka kanuni ya privacy,yeye aliomba kusaidiwa baada ya kuona mnamtelekeza,hoja ya msingi kwa nini yeye ndio akubaliane na mwenye nyumba kama kweli nyinyi mnakodisha kwa niaba yake?msitufanye wajinga,gari mara mbili kwa wiki ambalo mnamwambia linatengenezwa?inashindikana nini TSN kumtafutia nyumba toka shirika la nyumba la taifa?huu ni uzembe na kama kawaida kutojari waajiriwa wenu,kama kuna mwenyekiti wa hiyo TSN,na mkurugenzi basi hao wana mikono na roho za chuma,unawezaje kumfanyia mwenzenu mambo hayo bila kujali utu?shirika la umma na ni watu wangapi wanapata matatizo kama haya?na wafanyakazi wa TSN mnaweza changisha harusi za mamillioni mnashindwaje kumchangia mwenzenu ili maisha yake yawe ya kawaida??nawakilisha kwa wadau hii sio taarifa tuliyotarajia na imechukua siku kadhaa kujibu tuhuma hizi kweli hii ni haki??

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2012

    Kwa huduma zote anazopewa ni hii kampuni hastahili hata kidogo kulalalamika. Awe mwingi shukrani.

    ReplyDelete
  5. Athmani hakuzungumzia kua hakuhudumiwa kipindi alichopata ajali,alieleza yote aliyo saidiwa kipindi chote alipokua anaugua,hizo hesabu mnazotuletea kua mlimuhudumia kwenda huku au kule,ilikua ni haki yake,wala hajakanusha, msilete stori ndefu hapa, jamaa alicholalamikia nikwamba kua sasa mmesha anza kunuona amekua mzigo kwenu,hivyo mnataka kumchovyeka aingie mkataba na mwenye nyumba,yaani atie signature ya mkataba,mwisho wa siku mumkane,sasa janja yenu kaishtukia mnaanza kuleta habari ndeefu,muhudumieni, ni haki yake,hajapoteza akili,anachokiongea kama muandishi anajua mazara yake ikiwa anaongopa,mpeni haki yake mlemavu huyu. Mdau Tottenham London

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2012

    TSN hawajazungumzia kuhusu kubadilisha mtu wa kusaini mkataba kama ni wao au Hamisi, hiyo ilizungumziwa, hata kama mmetumia bilioni kumhudumia bado aliumia kazini, na mna bahati ingekuwa nchi za nje mngelipia na stress aliyopata na ndugu zake wangelipwa kwa stress waliopata, TSN wanaonyesha waziwazi wamemchoka, mhudumieni mpaka mwisho mnashangaa kwani ajali asingepata kama msingemtuma kikazi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2012

    Achani kuhukumu tsn au Athumumani maana nimeona wachangiaji mlio wengi mawazo yenu yapo biased.jengeni hoja,hivi ni wangapi wafanya kazi wa serikali hii hii ambao wamepata matatizo kama haya ya ugonjwa wakapangiwa nyumba na mwajiri?kwenye mkataba wake lipo suala la nyumba?nyumba nayo nisehemu ya matibabu?
    Mimi sijui watu wa sheria watusaidie nani hasa anapaswa kumlipia nyunba huyu bwana mkubwa.au sababu yeye mtu maarufu?mkata majani na yeye akiugua kama anaishi goba atapangiwa nyumba upanga ili iwe rahisi kwenda Muhimbili?

    MHINA

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2012

    If TSN account is true, then they have done more than enough.In the so called "developed world", one needs to have life insurance (with a clause about injuries) to get such treatment.No employer would incur any expenses towards its employee after such a tragic accident (In ughaibuni).
    Dr Gangwe Bitozi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2012

    TSN wamefanya vyema kuyaweka yote hadharani. Pamoja na Bw Athumani kutoa shukrani kwa huduma aliyopata kutoka kwa mwajiri wake na Serikali bado alionesha wanastahili kufanya zaidi. Taarifa hii imeonyesha kumbe wanafanya hivyo! Lakini kunafundisho hapa. Mwajiri yeyote hana jukumu lisilo na kikomo la kumhudumia mfanyakazi wake. Waajiri wawe na bima za wafanyakazi zinazotosheleza. Aidha watumishi nao waelewe kwamba kuna mambo yako nje ya uwezo wa mwajiri. TSN wamejitahidi hata zaidi ya jukumu lao kama mwajiri. Wanastahili pongezi na sio simanzi!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2012

    Personally nakiri TSN wamefanya kazi kubwa. Lakini kazi yenu kubwa hailingani na yeye kupata ulemavu wa maisha. Hawezi tena kabisa kumudu shughuli za utafutaji.

    Kwa nini hata kama mnaona matumizi yanakuwa makubwa , muione hii kama changamoto ya Corporate and Social Responsibility? Sahau mchango wake kwenu lakini muione hii kama tatizo ambalo mnaweza kusaidia? Kama mmeweza kugharamikia yote kwa nini msifanye hata utaratibu wa kumjengea kajumba atleast yenye gharama ya milioni 50?? fanyeni jithida za kutoa mpango wa kudumu.. Pole sana bwana athumani.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2012

    Duuh WACHANGIAJI hata hivyo mi nimejaribu kuangalia kwa jicho la TATU,hii kampuni si ya kuuza MAGAZETI jamani,,,,,,,wallaaah mtasikia muda si mrefu inaishia KABURINI,kwa gharama hizi WAMEJITAHIDI sana sio siri,na ndugu yetu MPIGANAJI alione hili,anaweza kubadili utaratibu wa maisha japo kidogo,kama alivyosema wafadhili wanaanza KUMKIMBIA,na ye ajaribu kujibana japo kidogo,kwa mfano watoto wanasoma shule ya laki 2 kwa term moja,term zenyewe ni 4 kwa mwaka,anaweza kutafuta ya ANGALAU kidogo,,,,ni hayo tu mawazo YANGU

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2012

    Lakini anategemea kuhudumiwa hadi lini! mie naona familia yake sasa ingeanza kuamka na kutafuta namna, sababu ni wengi wanaopata ajali makazini na hawapati huduma hio, ashukuru hapo alipofikishwa, na ajaribu kuishi maisha ya mtu wa kawaida sasa, kwani mbeleko inayombeba inaelekea kukatika.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2012

    Hapa mchonganishi anyempa maneno huyu jamaa,naamini TSN wanafanya lile linalostahili,na kama mshahara anaendelea kupata kila mwezi,aisee ni kushukuru sana.Aachane na MTU KATI hao ndo wanampa maneno ya kumchanganya!!wanataka wale cha juu!!asante TSN!mhudumie kwa kadri inavyowezekana!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2012

    Hapa tusishangae,unajua mtu ukiumwa kwa muda mrefu inafika mahali akili inakuwa haiko sawa.Ndugu yetu huyu kuna watu wanamchanganya,ndo maana ulisikia analalamikia ndugu na marafiki kumkimbia,kikubwa akubali huu ulemavu au ugonjwa aloupata ila awe na imani vile vile kwamba atapona.Tumezoea hapa kwenye misiba watu wanapata dili kupitia shughuli za misiba,nina wasiwasi hata huyu ndugu yetu kuna MADALALI wanaojifanya wanajua sheria wajua siri za kila kona hivyo wanamjaza maneno ili wapate mkate wao wa kila siku!!Kaka wasikuchanganye shukuru TSN wanaendelea kukulipa mshahara na huduma nyingine,una bahati sana,Achana na maneno ya vijiweni sijui UNGEKUWA ULAYA UNGE....,UNGE....!!!! hapa ni afrika na tanzania haya ndio maisha yetu.MUNGU AKUTIE NGUVU NA AKUWESZESHE KUWAONA HAO WANAOTAKA KUSHIBA KUPITIA HUO UGONJWA WAKO.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2012

    hujafa hujaumbika kwa kweli ,,kama alivyosema mwenyewe hakutegemea kama yatamkuta haya lakini yametokea ,,mimi ninalipongeza sana swala la mwenzangu hapo juu ajengewe nyumba angalau ya kawaida ya kuweza kujimudu yeye na family,,kwa mana hii pesa ya kumpangia ingeweza kumjengea na garama za TSN kupungua kidogo.watu wengi wanatoa comment according the way they think lakini chukua hili tatizo kama lingekukuta wewe.usiringe unatembea na unaviungo vyote ,,tukae na tumshukuru MUNGU kwa mana leo tunalala wazima hatujui kama kesho tutaamka au la ..

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 09, 2012

    Huyu jamaa amekuwa mlemavu wa ajali pole sana! kinachotakiwa hapa ni sheria za ajira zifuatwe bila kujali ni kwa huyu jamaa yetu au mtu mwingine! Kila Mtanzania anastahili haki kulingana na Katiba ya nchi. TSN hawatakiwa kusema wamemsaidia huyu ndugu maana wanatakiwa watimize yale yanayotakiwa kisheria. Huyu ndugu anatakiwa kudai ambacho anastahili kisheria kama kuna la ziada analohitaji anaruhusiwa kuomba kutoka TSN au taasisi yoyote na hata watu binafsi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 09, 2012

    Bima, jamani, Bima ni kitu muhimu, wote tunailamu hiyo kampuni yake bure tu. Wafanyakazi wakatiwe Bima ambazo ndio zitadeal na haya mambo. Huyo aliyesema sijui kampuni imlipe sijui stress sijui nini nafikiri haelewi hata hao wanaolipwa majuu ni pesa za Insurance ambayo mwajiri wako anakuwa amekata na hazitoki mfukoni mwake. Na isitoshe wenzetu serikali zao zina system ya kuwaangalia walemavu, kwa hiyo Athumani automatically angeingizwa kwenye benefit system serikali ikamtunza kama inavyowatunza walemavu wengine, sio peke yake. Umechelewa kidogo tu ungehamia UK kabla yaani nyumba ya bure, gari na monthly allowance pamoja na carer wako wangelipwa na serikali wakawa wanakuja kila siku kukuhudumia nyumbani kwako!

    Tena kuna watu hapo Bongo wameugua wakiwa kazini na hata miezi 6 haikufika wakafukuzwa kazi. Kuna kaka mmoja alikuwa dereva Songas miaka mingi ghafla akaumwa miguu akiwa kazini huko Rufiji, ikabidi dereva mwingine akafuate gari akarudishwa Dar, alihangaika peke yake na familia yake, na baada ya miezi 6 wakamuachisha kazi bila chochote. Kisha leo unamuona Mkurugenzi wa Songas kwenye magazeti anachangia $10,000 kwa elimu sijui nini. Shukuru Mungu Athumani hao TSN wamekuhudumia muda wote huo.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 09, 2012

    TSN mnakuja kama zimamoto sasa.. Mnavyojieleza na kujitetea jinsi mnavyomsaidia Athumani, basi Athumani atakuwa punguani kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia adha anazozipata na maisha yake kwa sasa na tena publicly ambayo hizo ni habari binafsi.. Hatua iliyochukua inaonyesha he was giving up on TSN..and it was his possibly last attempt to try and keep afloat..Na hii inaonyesha kuwa TSN mlianza kuonyesha kwa vitendo au maneno kuwa mmeanza kumtelekeza. Na ndio maana akaanza kutafuta njia mbadala za kuomba wasamaria wema wamsaidie. TSN hamuhitaji kusema pesa kiasi gani mmemsaidia Athumani kwani hiyo ni immaterial given ulemavu aliopata sasa, ambao huwezi kuthamanishwa na kitu chochote. Ni vizuri sasa mmejieleza kuwa hamjamtelekeza, whether that is the truth or not mtekeleze yale ambayo ki-utu mnatakiwa kumfanyia ndugu huyu na tena kwa vitendo si kwa maneno tu..

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 09, 2012

    Mwenyezi Mungu ana mipango yake kwa kila jambo,saa ingine dhana ina dhambi lakini mungu atusamehe,mie naona aidha ndugu wanataka huyu bwana awe kitega uchumi,kwani huo msaada wameona ni mdogo hivyo basi mchango aliofanyiwa Sajuki ni mkubwa naona anataka ifanyike hivyo ili baadhi ya ndugu wanufaike na huyo bwana Hamisi,na wazo la bima jamani ni muhimu sana kwani leo tunavyokatwa nssf ni kwa ajili ya msaada wa maisha yako hapo baadae,hali kadhalika bima ni msaada mkubwa wa matatizo ambayo unaweza ukachaguakama ni ajali au ukiugua na kadhalika ziko aina nyingi, na pia serikali ilazimishe watu waingie kwenye bima wakatwe kwenye mishahara kama nssf.
    Hili ni wazo langu nawe changia la kwako,sio tubishane pasi na tija.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 09, 2012

    ajengewe nyumba tu story hazi saidii.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 09, 2012

    watanzania wanapenda vya bure wawe wazima au wakiugua. Hiyo wanaona haki yao. Mtu anaumwa kidogo tu siku tatu analala nyumbani anajua mshahara upo serikali inapoteza pesa nyingi kwa huruma kama hizi, hilo watu hawalioni. Wagonjwa wa ukimwi ni wengi makazini na wao huwa wanaugua muda mrefu wanapata mishahara. Sheria inatoa miezi ya mshahara, baada ya hapo ni half salary, ikizidi hapo ni kuachishwa kazi, sheria na kanuni ziko wazi. Vipi nyinyi.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 09, 2012

    Navyojua ikiwa mfanyakazi kapata ajali kazini ni jukumu la mwajiriwa kumhudumia, hapa kwetu Tanzania hizi sheria ziko wazi na zinaeleza mipaka yake ila tatizo la waajiri wetu wao hawapendi ziwe wazi na wanachukulia ni kama fadhila pindi pale wanapotekeleza na serikali yetu haiko kutetea wafanyakazi hata kidogo.
    TSN hata kama mlikuwa mnamlipa kiasi kidogo ukilinganisha na gharama mlizotumia sasa na mshahara wake tofauti ni kubwa sana,kumbukeni ulemavu aliopata ni pigo kubwa kwa jamii yake,kuna watu wengi nyuma yake waliokuwa wanamtegemea si kifedha tu hata nguvu kazi, na sasa inabidi yy ahudumiwe. Asingefanya kazi siku hiyo hayo yote yangetokea!? lakn juhudi zake za kujitoa kupenda kazi yake ndiyo iliyomfikishia hapo.Nashauri liangalieni hili swala kwa mtazamo tofauti kurushiana maneno huyu hajanisaidia...huyu nimesaidia...haileti mantiki muhimu hapa ni kuwa Hamisi ameonyesha anaitaji msaada toka kwenu na itafutwe njia mbadala ambayo mkimsaidia leo kesho anaweza akaja kusimama na kusema kweli TSN wamenisaidia na kwa sasa siitaji tena msaada wao.siyo kila siku mnapeleka msaada ambao mnajua kesho lazima ataitaji tena msaada ili muonekane kweli mnajali ila kiukweli hamtaki kufikiri.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 09, 2012

    Msiongee kwa kufuata mioyo inavyowambia. Kuweni objective. SHeria inasemajeee? Kuwa ukipata ajali kazini ujengewe nyumba??? Mi nadhani kumpa mshahara bila kumkata kwanza ni favor. Hivi serikali ikianza kujengea watu nyumba pindi wapatapo ajali nchi hii itafika kweli. Kumbuka akifanyiwa Athumani na Rehema pia au Joseph nae atadai kwani itakuwa ni precedence. Tumieni vichwa kufikiri si mioyo.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 09, 2012

    TSN mmejitahidi sana na ni haki yenu kuweka hii defence ili watu waelewe kwani bila ya taarifa hii kuwekwa hadharani basi tayari dignity na reputation yenu tayari ilikuwa imeshaharibika. Mnastahiki kupongezwa kwa kweli.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 09, 2012

    TSN mmejitahidi sana na ni haki yenu kuweka hii defence ili watu waelewe kwani bila ya taarifa hii kuwekwa hadharani basi tayari dignity na reputation yenu tayari ilikuwa imeshaharibika. Mnastahiki kupongezwa kwa kweli.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 10, 2012

    Naomba kuuliza maswali yafuatayo:

    1, sheria inasemaje kuhusu kuumia kazini

    2, aina za kuumia kazini ni zipi

    3, ajali kazini, mwenye kosa ni mwajiri au aliyesababisha ajali? kama ni aliyesababisha ajali, bima yake ndio ihusike? ama?

    4, je, ni haki ya kila mwajiriwa kutibiwa milele, kulipiwa kodi ya nyumba milele, na kulipwa mshahara kamili milele?

    5, je, kuna wafanyakazi wangapi wa serikali sasa hivi, ambao waliumia kazini, ambao:
    a, wanalipiwa mshahara kamili milele
    b, wanalipiwa kodi ya nyumba milele

    Nikijibiwa haya, naweza sasa kuchangia rasmi hii mada

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 10, 2012

    mie nadhani TSN imefanya ziada, kwasababu angekuwa bado anafanya kazi asingepata mshahara kamili, angekuwa analipa kodi pia. Mshahara anopewa huyu bwana unamtosha kuendesha maisha yake na familia yake. TSN mmefanya zaidi ya aliyostahili, kwa mtazamo wangu naona huyu jamaa hana shukrani, na kama kuna mtu anamdanganya atakujakujuta. Alistahili kupata mshahara kamili within six month, then nusu mshahara na baadae aachishwe kazi, hivyo ndivyo ilivyo kisheria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...