Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud amesema nchi yake imeamua kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa ya Tanzania katika ununuzi wa bidhaa za afya na kubadilishana uzoefu wa namna mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya unavyofanya kazi.

Rais Mahamud ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, ameyasema hayo alipoitembelea MSD, na kuongeza kuwa kutokana na uzoefu wa MSD, wana uhakika kuwa ubora wa bidhaa za afya utakuwa wa uhakika.

Naye Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ameeleza kuwa kwa kuwa sasa Somalia ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania kupitia MSD itaweza kununua bidhaa za afya kwa pamoja ili kupata bidhaa hizo kwa bei nafuu.

Ameongeza kuwa, Marais wa nchi hizo mbili, yaani Tanzania na Somalia wamewapa maelekezo Mawaziri wa Afya nchi zao kukaa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana katika masuala ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwa urahisi, kuzingatia ubora na kwa bei nafuu.

Kiongozi huyo wa Somalia na ujumbe wake alizungumza na viongozi wa Wizara ya Afya, Menejimenti ya MSD na kutembelea ghala la kuhifadhia dawa la makao makuu MSD.






Dar es Salaam. Tarehe 27 Aprili 2024: Katika kuunga mkono juhudi za kuboresha elimu nchini, Benki ya CRDB imeasaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha Wawekezaji katika Elimu Tanzania (TAPIE) utakaowawezesha wanachama wake kupata mikopo nafuu ya kuboresha miundombinu na kuwezesha uendeshaji wakati wote.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 27 Aprili 2024 kwenye mkutano mkuu wa 5 wa mwaka wa TAPEI uliofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt Doto Biteko na kuhudhuriwa na wadau wa elimu nchini.
Akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu huo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa amesema Benki inatambua changamoto wanazokutana nazo wamiliki binafsi wa shule hivyo imechukua hatua za kusaidia kuzitatua ili kuwa na mazingira rafiki kwa wanafunzi kusoma na kujifunza.

“Ni ukweli usiopingika kuwa elimu ndio msingi wa maendeleo ya Taifa lolote lile duniani kwani husaidia kujenga maarifa, ujuzi na kuongeza ufanisi hivyo kuwa kichocheo muhimu katika ukuaji wa uchumi. Kwa kuyatambua haya yote, Benki ya CRDB imeiweka sekta ya elimu katika moja ya vipaumbele vyake vya uwezeshaji. Tunafanya hivi ikiwa ni sehemu za kusaidia jitihada za Serikali pamoja na wadau wa sekta hii kutoa elimu bora itikayozalisha rasilimali watu bora katika nyanja mbalimbali,” amesema Raballa.

Kwa kuzitambua changamoto zilizopo ukiwamo ukweli kwamba uendeshaji wa shule unategemea mapato yatokanayo na ada ambayo mara nyingi hukusanywa shule zinapofunguliwa hivyo kuwa na uhaba pindi zinapofungwa, Benki ya CRDB imewaletea mkopo wa uendeshaji ili kukidhi mahitaji yanayopaswa kulipiwa wakati mapato mengine yakisubiriwa indi muhula mpya utakapoanza.
Raballa pia amesema shule nyingi zipo kwenye maeneo ambayo hayajarasmishwa jambo linalowanyima wamiliki uwezo wa kukopa kutokana na kutokidhi vigezo vya dhamana hivyo Benki ya CRDB imewaletea suluhisho kwa kuwaruhusu kukopa fedha zitakazowezesha urasmishaji wa maeneo yao ili kupata hati ya wizara itakayowaruhusu kukopa ili kuimarisha biashara zao.

“Tunawaruhusu wamiliki wa shule kukopa mpaka shilingi milioni 10 kwa ajili ya kurasmisha maeneo ya shule. Fedha hizi ni kwa ajili ya kutafuta hati ya wizara hivyo kuyatambulisha maeneo yao ya kisheria. Vilevile, tunayo mikopo kwa dhamana zisizo rasmi yaani maeneo ya shule ambayo hayana hati. Benki yetu inamruhusu mmiliki kuja kukopa mpaka shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya shule. Tunaamini kwa utaratibu huu rahisi na rafiki, tutasaidia kuwezesha uwekezaji wa shule katika sekta binafsi,” amesema Raballa.
Wakati wamiliki wakipewa mkopo wa uwekezaji wanaoweza kuurejesha mpaka kwa miaka 7, Raballa amesema walimu na wafanyakazi wa shule binafsi nao wanaweza kupata mkopo kwa ajili ya kufanikisha mambo yao binafsi. Mikopo ya wafanyakazi hawa, amesema inajumuisha ‘salary advance’ ambao ni mahsusi kwa wale ambao mishahara yao inapitia Benki ya CRDB ambao wanaweza kupata mpaka asilimia 50 ya mshahara wao na wakalipa ndani ya siku 30 pamoja na mkopo wa binafsi unaofika mpaka shilingi milioni 100 zinazoweza kurejeshwa kwa mpaka miaka 8. 
 
”Kwa miaka mitatu iliyopita, kiwango cha mikopo ya eimu tuliyoitoa kwa kundi hili imekuwa ikiongezeka. Mwaka 2021 Benki yetu ya CRDB ilikopesha zaidi ya shilingi bilioni 78.66 ambazo zilipanda mpaka shilingi bilioni 86 mwaka 2022 na mwaka jana zikawa shilingi bilioni 97.17. Nitumie fursa hii kuweka wazi kwamba mikopo hii tunayotoa kwa wamiliki wa shule binafsi hasa wanachama wa TAPIE, inaweza kurejeshwa mpaka kwa miaka 7,” amesisitiza Raballa.

Kwa upande wake, rais wa TAPIE, Mahmoud Mringo amesema hadi sasa kuna zaidi ya shule 6,362 zinazojumisha za awali 2,364, za msingi 2,270 na sekondari 1,728 zinazomilikiwa na watu binafsi, mashirika ya dini na yasiyo ya dini, majeshi, na jumuiya za wazazi ambazo zimedahili takriban wanafunzi 1,020,772 kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita ambazo zimeajiri takribani walimu 59,445 na wataalamumwengine zaidi ya 100,000 wenye taaluma na ujuzi mbalimbali kama wahasibu, madereva, wasimamizi na walezi wa wanafunzi, walinzi na wapishi. Ajira hizi zimesaidia kuinua hali za kimaisha kwa watu husika na kupanua wigo wa kodi mbalimbali na hivyo kukuza uchumi wa taifa.

“Ukitaka kujenga darasa, maabara au kuboresha miundombinu mingine ya shule, ni lazima uende kukopa benki lakini tatizo ni riba kubwa. Kujenga shule ndogo tu kwa sasa unahitaji walau shilingi bilioni 2 lakini kuwa na shule yenye kila kitu basi unahitaji shilingi bilioni 10. Ukizikopa hizi kutoka benki na ukalipa kwa riba iliyopo, itakuchukua miaka 20 ya kumaliza deni ambalo ni lazima lilipwe na mwanafunzi. 
 
Bado kuna kodi na tozo 16 ambazo shule inatakiwa kulipa. Haya mambo yote yanaifanya elimu yetu kuwa ghali na kusoma shule zisizo za serikali inaonekana ni anasa,” amesema Mringo akiiomba serikali iangalie namna ya kupunguza riba ya mikopo tozo pamoja na kodi.
Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko amepongeza juhudi za sekta binafsi kuchangia kuboresha elimu nchini kwamba zinaifanya jamii iwe na mchango zaidi katika kukuza uchumi. "Niwapongeze kwa ushirikiano na mkataba wa makubaliano mnayosaini leo na Benki ya CRDB. Ili kufanikisha mambo, ushirikiano na wadau wengine ni muhimu sana. Hivi mnavyofanya, ndio namna nzuri ya kukabiliana na changamoto zetu," amesema Dkt Biteko.



 


Meneja Uhusiano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Shule ya Sekondari ya wasichana Kilakara aliyekuwa anafanya vizuri kitaaluma. kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mary Lungina. Mahafali yao yamefanyika leo shuleni hapo Mkoani Morogoro.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa uhusiano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa akiwa na viongozi wa shule na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana Kilakala katika meza kuu wakati wa mahafali ya kidato cha sita shuleni hapo.


Baadhi ya wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunikiwa vyeti.

KAMPUNI ya dhahabu ya Barrick nchini, imeeleza dhamira yake yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini ikiwemo kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi na TEHEMA mashuleni ili taifa lisibaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi ya teknolojia.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Barrick Tanzania, Georgia Mutagahywa katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kilakala, iliyopo mkoani Morogoro ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.

Alisema tayari Barrick imeanza kutoa hamasa na motisha kwa watoto wa kike wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri katika somo la hisabati na kutoa wito kwa wasichana kujiamini, kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu na kuondoa dhana ya kwamba masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana.

Katika jitihada za kuunga mkono jitihada za Serikali, Barrick kupitia mpango wake wa ya Kusongesha Mbele Mustakabali wa Elimu, iitwayo “Barrick-Twiga Future Forward Education Program” imetoa dola milioni 30 , (takriban shilingi bilioni 70.5 za fedha za Tanzania) kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya elimu nchini Tanzania kwa ushirikiano na Serikali.

Programu ya Barick-Twiga ya Kusongesha Mbele Mustakabali wa Elimu, iitwayo “Barrick-Twiga Future Forward Education Program” inalenga kufanikisha ujenzi wa madarasa 1,090, majengo ya maliwato na vyoo 1,640 na mabweni 270 katika shule 161 nchini kote ili kusaidia kuwapatia malazi wanafunzi takribani 49,000 katika sekondari za masomo ya juu (A-level).

Kwa upande wake,Mkuu wa shule hiyo Mary Lungina,aliishukuru Serikali na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia kuunga mkono jitihada za kuinua kiwango cha elimu nchini na alitoa rai kwa wahitimu kuongeza bidii katika kutafuta elimu zaidi ili iwasaidie katika maisha yao sambamba na kujenga Taifa.
Rais wa Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud akitazama chumba cha upasuaji kilichowekwa mtambo wa matibabu ya moyo ‘Cathlab’ katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar Es Salaam leo Aprili 27, 2024. Rais H.S Mohamud amepokelewa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.




Na WAF – Dar Es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuanzisha Taasisi mahususi ambayo itakuwa inashuhulikia masuala ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ili iweze kuboresha zaidi huduma hizo za ubingwa kuitoa katika Taasisi ya Mifupa Ubongo (MOI) ambapo itabakia na masuala ya upasuaji wa mifupa pekee.


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Aprili 27, 2024 baada ya uzinduzi wa chama cha madaktari bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu (Tanzania Neurosurgical Society) kikiongozwa na Rais wa chama hicho Dkt. Othmani Kiloloma Jijini Dar Es Salaam.


“lengo la chama hichi ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora na salama za upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, ikiwemo upatikanaji wa madaktari bingwa wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu”. Amesema Waziri Ummy


Amesema, Tanzania kuna madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu 25 tu, ambapo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inapendekeza angalau katika kila watu 150,000 kuwe na daktari bigwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Mmoja.


“Ukichukua idadi ya madaktari bigwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu 25 tulionao maana yake kwa Tanzania daktari bigwa Mmoja anahudumia Watanzania Mil 2,400,000, huduma hizi bado hazijawafikia Waanzania wengi ndio maana chama hichi kimekuja ili pia kujengeana uwezo na kuhamasisha madaktari wengine waweze kusomea fani hiyo ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu”. Amesema Waziri Ummy


Aidha, Waziri Ummy amesema, Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kibingwa, usambazaji wa maafisa wa Afya katika vituo vyote vya Afya na Hospitali, uanzishwaji wa huduma za kina za upasuaji katika Hospitali za Rufaa za Kanda na ukuzaji wa wataalamu wadogo katika Hospitali za Rufaa za Mikoa.


“Lakini pia Serikali imeendelea kuweka msisitizo wa elimu endelevu katika taaluma za upasuaji ikiwa ni pamoja na upasuaji wa Neurosurgery, Neuro-radiology, Neuropathology, Neuro-anesthesiology, critical care, Neurology, pamoja na Neuro-rehabilitation”. Amesema Waziri Ummy


Pia, Waziri Ummy amesema Serikali imeendelea kuimarishwa upatikanaji mkubwa wa huduma za uchunguzi kupitia CT-scan katika Hospitali zote za Rufaa za Kanda pamoja na ujumuishaji wa huduma za MRI na huduma za ‘Angiography’ katika vituo vya ngazi ya juu ili kumrahishia Mtanzania kupata huduma hizo za uchunguzi ndani ya nchi.
Na Mwandishi Wetu
WAZAZI na walezi nchini wamesisitizwa kuacha tabia ya kuwatolea lugha zisizofaa watoto wao wanaofeli masomo na kuwaonesha kuwa hawawezi.

Rai hiyo imetolewa na Mwasisi wa Shule ya Sekondari Huria ya Skillful, Diodorus Tabaro wakati wa Mahafali ya 18 ya Kidato cha Sita, yaliyofanyika shuleni hapo Ukonga ambapo wanafunzi 75 wanatajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu.

Alisema ni vyema mzazi kutumia lugha rafiki kwa Watoto wanaofeli mitihani yao pamoja na kutafuta njia ya kumsaidia ikiwemo kumtafutia shule Huria aweze kuendelea kusoma ili kufikia malengo yake.

“Wazazi waepuke kuwanenea mabaya watoto wao. Kuna wazazi ambao mtoto wao asipofanya vizuri wanaongea nao kwa lugha hasi na kuwaonesha kuwa hawawezi, mdomo wa mzazi ambaye kijana wake anamuona yeye ndo baba au mama, unamuumbia mwanafunzi au kijana husika hivyo kupoteza hali ya kujiamini.

Akizungumzia kuhusu Shule Huria ya Skillful, alisema imefanikiwa kufaulisha wanafunzi 600 kujiunga na vyuo vikuu nchini kwa kipindi cha miaka 18 ya kutoa huduma.

Alisema idadi hiyo ya wanafunzi ni mbali na wale waliojiunga na Vyuo kwa ngazi ya Diploma au cheti na walioamua kujiajiri na kuendelea kutafuta maisha.

Tabaro alisema idadi hiyo kubwa imetokana na hali nzuri ya ufaulu wa wanafunzi wanaopita shuleni hapo ambao hakuna anayepata daraja la nne, isipokuwa kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu.

“Siri kubwa ya sisi kufanya vizuri na kupata wasomi wengi wa vyuo vikuu ni kutoa elimu bora inayomfanya mwanafunzi na mzazi wasijute kuchakua Skillful kwasababu hatutaki arudie kufeli tena mitihani,” alisema Tabaro.

Alitaja mbinu chache za shule hiyo kufanya vizuri kuwa ni walimu kuandaliwa kuwa wazazi, walimu na viongozi wa wanafunzi ili kuwasaidia wanafunzi kufikia malengo yao.

Mkuu wa Shule hiyo, Allen Maximillian amesema wanafunzi hao wanahitimu kwa kusoma kidato cha sita ndani ya mwaka mmoja katika michepuo yote ya Biashara, Sanaa na Sayansi.

“Tumekuwa na muendelezo wa matokeo mazuri ambao unachagizwa na jitihada za walimu, mazingira pamoja na nidhamu kwa walimu na wanafunzi,” amesema.

Aliongeza kuwa, mafanikio ya shule hiyo pia yanaenda sambamba na ushirikiano na serikali ambao wamekuwa wakiwasimamia bega kwa bega kuhakikisha elimu wanayotoa inakidhi vigezo.

Naye mmoja wa wahitimu hao, Derich Mushenyera, alisema wamejiandaa vyema kufanya mitihani ya mwisho ya kidato cha sita inayoanza wiki ijayo na anaamini watafaulu.

“Maandalizi yalikuwa mazuri, walimu wametufundisha mbinu za kufaulu lakini pia tumefanya mitihani ya mazoezi ya kutosha hivyo tunaamini tupo tayari kwa mitihani na kufaulu vizuri,” alisema.
Na Mwandishi Wetu, Arusha

WANANCHI wa Jiji la Arusha wakiwemo Baba na Mama Lishe wameishukuru Kampuni ya Oryx Gas kwa hatua inazochukua za kuhakikisha kundi hilo linatumia nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuharakisha shughuli zao sambamba na kuwaepusha na madhara yanayotokana na kutumia kuni na mkaa wakati wa kupika.

Wakizungumza leo Aprili 27,2024 wakati wa hafla ya kukabidhiwa mitungi ya gesi ya oryx na majiko yake 1500  yotolewa na Oryx kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo ambapo wajasiriamali hao wameeleza kuwa hatua hiyo ya kupewa mitungi ya gesi inakwenda kuwaondolea adha waliyokuwa wakiipata kwa muda mrefu.

Wajasiriamali Asha Mtumwa na Karim Abdallah wamesisitiza kuwa ni jambo la kupongeza kuona kampuni ya Oryx inawakabidhi mitungi hiyo kwani inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanzia kwenye afya pamoja na mazingira

Pia mitungi waliyokabidhiwa inakwenda kuwarahisishia shughuli zao kwa urahisi kutokana gharama nafuu ya gesi kuliko matumzi ya mkaa ambayo ni gharama na si rahisi kurahisisha kupikia.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka kwasababu ya kutumia nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.

Amesema hatua hiyo ya makabidhiano ya mitungi inakwenda kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi.

“Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa katika mazingira.

“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna uharibifu wa mazingira.Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 46242 zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dk.Jafo.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa kina mama na wasichana kwa asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.

“Leo hii ukiona nchi imejipanga katika nishati safi ya kupia ni jambo la msingi lenye kutia matumani.Watafiti  wanatuambia kitendo cha kutumia nishati safi ya kupikia kwa akina mama wajazito kunasaidia kurekebisha presha ya mama mjazito,”amesema.

Nae Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali katika jimbo hilo.

Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.

Vilevile kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman amempongeza Gambo kwa kuona umuhimu wa kuligusa kundi hilo kwa kuhakikisha linatumia nishati safi ya kupikia katika shughuli zao.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea madhara yanayotokana na kutumia kuni na mkaa ambapo amesema nchini  Tanzania, wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na gesi ya Oryx itatatua jambo hili.

Aidha amesema kupika kwa kutumia gesi ya Oryx huzuia ukataji miti, kwa hiyo husaidia kulinda mazingira huku akieleza pia  kutumia gesi ya Oryx huzuia wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa msituni.

"Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx ni kupika kwa haraka na kwa ufanisi zaidi; kwa hiyo, wanawake wataanda chakula kwa wakati na wanaume hawatalalamika juu ya kuchelewa kwa chakula kinachosababisha mizogo.

"Kwa hivyo, Oryx Gas Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza maono ya Rais kuhusu upatikanaji wa nishati.Namshukuru Mbunge wa Arusha Mjini Gambo na serikali ya Tanzania  kwa kutuunga mkono katika mipango yetu ya nishati safi kwa kuhakikisha matumizi ya gesi ya Oryx hapa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akiwasikiliza mama lishe na baba lishe kwenye hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Baadhi ya watumishi wa Kampuni ya gesi ya Oryx wakiwa katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 

Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Oryx, Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Oryx wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha  

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 

Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kulia),Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Haji Ussi (GAVU) (wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akiwa na watumishi wa Kampuni ya gesi ya Oryx wakiwa kwenye picha ya pamoja na mama lishe na baba lishe wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

 Na Mwandishi wetu

BAADHI ya wananchi wanaoishi katika Kijiji cha Endulen ndani ya Tarafa ya Ngorongoro wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kuwahamisha kwa hiyari kutoka kijijini hapo kutokana na kusumbuliwa na changamoto ya Wanyama pori wakali.

Wakizungumza katika zoezi la uelimishaji, uhamasishaji na uandikishaji baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa kasi ya ongezeko la wanyama wakali na waharibifu kama fisi, chui, Nyati, simba na tembo imewafanya washindwe kufanya shughuli zao za maendeleo na hivyo kuamua kuondoka kuelekea Msomera na maeneo mengine.

Wamesema hawaoni sababu ya kuendelea kuishi katika eneo hilo wakati kuna maeneo mengi nchini ikiwemo Kijiji cha Msomera ambayo yametengwa na Serikali na watu wanaishi kwa amani bila kusumbuliwa na wanyama wakali wanaokula mifugo yao ndani ya hifadhi.

“Humu ndani ya hifadhi hatuna amani yoyote hasa kutokana na kukimbizana na wanyama wakali, maisha ya humu ndani ya hifadhi yamepitwa na wakati ndio maana nimeamua kujiandikisha kwa hiyari na kuondoka kwenda katika Kijiji cha Msomera,”alisema Bi Maria Lepilal mkazi wa kijiji cha Endulen.

Wakazi wengine wa Kijiji cha Naiyobi ambao majina yao tunayahifadhi kutokana na sababu za usalama wao wamesema kadri wanavyokubali kuhama kwa hiyari wamekuwa wakipokea vitisho na hata kutengwa kutoka kwa baadhi ya wanaharakati wanaotaka zoezi hlo likwame kwa maslahi yao wenyewe bila kujali hali ya wananchi.

“Wanaharakati na baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitushawishi kubaki humu ndani ili waendelee kututumia kwa sababu zao za kiuchumi bila kujali shida tunazopata, mwezi uliopita boma la jirani yangu kundi la fisi waliingia wakalaa mbuzi 7, ndiyo maana tunaamua tukijiandikisha tuondoke ili tukaanze maisha mapya na kuepukana na adha ya kuishi ndani ya hifadhi kama wanyamapori,”alisema mkazi mmoja wa Kijiji hicho.

Vijiji vya Naiyobi, nainokanoka, Kapenjiro, Osinoni, Olpiro, Meshili na Esere ni miongoni mwa vijiji vilivyopo katika tarafa ya Ngorongoro ambavyo vimepokea zoezi la kuhama kwa hiyari kwa ari kubwa ambapo baadhi ya wanaharakati wanaotaka zoezi hilo likwame wameamua kuondoka na kuhamia maeneo mengine.

 

Tunakuletea mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa fursa ya kukusanya vito na madini. Ikiwa unakusanya kwa wingi, utapata ushindi wa ndoto zako kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Fanya Kujisajili Meridianbet Ufurahie bonasi za kasino, promosheni, na mizunguko ya bure

Jinsi ya Kucheza Mega Jade Kasino.

Mega Jade ni sloti ya kasino ya mtandaoni kutoka kwa mtoa huduma Red Tiger, mchezo huu una safu tano zilizowekwa katika mistari mitatu na ina mistari 10 ya malipo ambayo haiwezi kubadilishwa. Ili kushinda, lazima uunganishe alama tatu au zaidi kwenye mstari wa malipo.

Mchanganyiko wowote wa kushinda unalipwa kwa pande zote mbili. Iwe unashinda kutoka kushoto kwenda kulia au kulia kwenda kushoto, utalipwa sawa. Na bora zaidi, mstari wako wa ushindi hautalazimika kuanza na safu ya kwanza kushoto au kulia.

Wkati unacheza mchezo huu wa Kasino ya Mtandaoni unaweza kupata ushindi mmoja kwa kila mstari wa malipo. Ikiwa una mchanganyiko wa kushinda zaidi ya moja kwenye mstari wa malipo, utalipwa ushindi wa thamani kubwa zaidi.

Inawezekana kukusanya ushindi kwa kuwaunganisha kwenye mistari ya malipo zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Kwenye sehemu ya Stanje, kuna vitufe vya "plus" na "minus" ambavyo unaweza kutumia kuweka thamani ya dau kwa kila mzunguko.

Pia kuna chaguo la kucheza moja kwa moja ambalo unaweza kulianzisha wakati wowote. Kupitia chaguo hili, unaweza kucheza hadi mizunguko 100. Kabla ya kuanzisha chaguo hili, weka kikomo cha hasara kinachostahimiliwa.

Ikiwa unapenda mchezo wa haraka zaidi, Meridianbet wana suluhisho kwako. Weka mizunguko ya haraka kwa kubofya kwenye sehemu iliyo na lebo ya Turbo. Unaweza kudhibiti athari za sauti kwenye kona ya juu kulia juu ya safu.

Alama za Ushindi Mega Jade

Kuhusu alama za mchezo huu, zimegawanywa katika makundi kadhaa kulingana na thamani yao ya malipo. Kwa kawaida, alama za kadi ndizo zinazolipa malipo madogo, lakini pia zimegawanywa katika makundi mawili.

Alama za kadi za 10, J, Q zinatoa thamani ndogo zaidi ya malipo. Ikiwa unaunganisha alama tano hizi kwenye mstari wa malipo, utapata mara 10 ya dau lako.

Moja kwa moja baada yao, kuna alama zingine za kadi: K na A, lakini kunaongezewa na kito cha kijani ambacho kinatoa malipo sawa. Ikiwa unaunganisha alama tano za hizi kwenye mstari wa malipo, utapata mara 20 ya dau lako.

Mwamba wenye umbo la octagon ni alama inayofuata kwa thamani ya malipo na inatoa nguvu kubwa ya malipo. Ikiwa unaunganisha alama tano za aina hii, utapata mara 30 ya dau lako.

Moja ya alama zenye thamani kubwa zaidi ni mwamba wenye umbo la hexagon na fremu ya dhahabu karibu nayo. Ikiwa utaunganisha alama tano za hizi kwenye mstari wa malipo, utapata mara 50 ya dau lako. Tumia nafasi hii na upate ushindi mzuri.

NA WILLIUM PAUL, SAME. 

MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wananchi wa kata ya Ruvu kuwa makini na maji yanayotapakaa katika maeneo hayo kutoka mto Ruvu kutokana na maji hayo kuja na mamba ambao wanaweza kuleta madhara kwao. 

Mkuu huyo wa wilaya pia amewaagiza Tarura kufika katika kata hiyo na kuona jinsi watakavyoweza kufungua njia ambapo kwa sasa maji yametapakaa kila mahali hali inayiwalazimu wananchi kutumia mitumbwi kutoka kwenda kutafuta mahitaji yao.

Kasilda amewataka kuacha kufanya shughuli za uvuvi wa samaki kiholela katika maeneo hayo kwani mamba hao wamekuwa wakiwakimbiza wananchi ambapo mpaka sasa Mwananchi mmoja ameshauwawa. 

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Ruvu, Yaigongo Mrutu amesema kuwa eneo kubwa la kata hiyo limezungukwa na maji yakiwamo mashamba ambapo kwa sasa wananchi hawajui hatima yao. 




Top News