OMBAOMBA MAARUFU NCHINI, MZEE ANTHONY MATONYA, AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA KIJIJI CHA BAHI, KITONGOJI CHA NGHUNGUNGU,  MKOANI DODOMA.  
MWILI WAKE UNATARAJIWA KUZIKWA KATIKA MAKABURI YA KITONGOJI HICHO MAJIRA YA SAA 10 JIONI KIJIJINI HAPO. 
TAARIFA ZAIDI ZITAENDELEA KUTOLEWA KADIRI ZITAKAPOTUFIKIA
GLOBU YA JAMII  PAMOJA NA MTANDAO WA JUMA MTANDA TUNATOA MKONO WA  POLE KWA NDUGU, JAMAA NA MAFARKI KWA MSIBA HUU MZITO AMBAO TUTAKE TUSITAKE NI WA TAIFA ZIMA.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI 
AMIN
http://3.bp.blogspot.com/_mnq0IaLJvsI/SClRcvDRC4I/AAAAAAAABis/KqTFTzZpmi4/s400/MATONYA%2520PIX%2520NO%25201%2520%25281%2529%5B1%5D.JPG
Picha za matukio za ombaomba maarufu Mzee Anthony Matonya enzi za uhai wake katika eneo la daraja la mto Morogoro wakati akiwaomba samaria wema kuweza kumsaidia pesa kwa ajili ya kujikumu wakati huo akiishi katika kambi ya wazee ya Funga Funga Kichangani Manispaa ya Morogoro kati ya mwaka 2009 na mwaka 2011 kabla ya kurejea kwao katika Kijiji cha Bahi Sokoni, Kitongoji cha Nghungugu mkoani Dodoma. 



Picha za matukio za ombaomba maarufu Mzee Anthony Matonya enzi za uhai wake katika eneo la daraja la mto Morogoro wakati akiwaomba samaria wema kuweza kumsaidia pesa kwa ajili ya kujikumu wakati huo akiishi katika kambi ya wazee ya Funga Funga Kichangani Manispaa ya Morogoro kati ya mwaka 2009 na mwaka 2011 kabla ya kurejea kwao katika Kijiji cha Bahi Sokoni, Kitongoji cha Nghungugu mkoani Dodoma.  

Picha zote za maktaba na habari na www.jumamtanda.blogspot.com 
 Kupata mwandani wa Hayati Mzee Matonya BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Kifo cha huyu mzee matonya kimenisikitisha sana kwa kweli serikali yetu inatia aibu sana

    roho mbovu za viongozi tulionao huyu mzee amekuwa ombaomba takribani umri wake wote mpaka kifo kimemchukua hakuweza kupatiwa msaada wowote na serikali

    marehemu mzee matonya ni mtanzania halisi ambae nchi yake ina utajiri mwingi wa madini misitu na maliasili nyingi tu

    mzee matonya amefariki dunia bila kupata raha ya kula matunda ya nchiyake kama walavyo mafisadi na viongozi wengi wabinafsi

    Kifo cha mzee matonya kinasomeka na kina mtazamo wa kila mtanzania mwenye hali ngumu ya kimaisha atakufa bila kufaidika na msaada wowote unaotokana na uwezo utajiri asilimali za nchi yake

    Mungu ilaze pema roho ya huyu masikini wa duniani umjaalie awe tajiri wa paradiso.ameen

    ReplyDelete

  2. "Tutake tusitake ni wa Taifa zima" ?????!!

    Sio kwamba namdharau ombaomba but HOW !!!

    Kivipi yani??

    ReplyDelete
  3. Michu, aaa !! bwana ,mbona ya leo kali ??? imekuwa vyema kwamba umeiweka kwenye kiswahili ,maana duh !!! mimi kwa kuelewa kwangu ni kwamba ,msiba wa Taifa ni kwa mtu yule ambaye amelifanyia kazi Taifa lake na kuliletea manufaa fulani.Wengi wetu ,bado hatujafikia hata hiyo robo ili kupata hiyo heshima ya ( msiba wa Taifa) kama tunakufa leo au kesho. WEWE Ankal ni tayari umeshaingia kwenye heshima hiyo, ukifa leo, Lazima barabara zifungwe. Sasa huyu ombaomba jamani!!! kaifanyia nini nchi yake ???? Mungu ailaze pazuri roho yake huko peponi.( amina) Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  4. R.I.P Matonya!

    Je taarifa za Msiba huu amefikishiwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Lt. Matsafu Mzee Yusuf Makamba?

    Maana Makamba alikuwa mtani mkubwa wa merehemu Matonya.

    Alikuwa anaburuzana naye sana Jijini kuhusu kumrudisha Kijijini Dodoma pana siku Makamba alihakikisha anafikishwa Kijijini chini ya Maafisa wasimamizi lakini siku ya tatu Makamba akakumbana na Matonya Dar!

    ReplyDelete
  5. Che GUevaraAugust 25, 2012

    RIP Matonya1

    BUT kwanini karibu ombaomba wote hapa NCHINI ni WAGOGO? na wapo katika mikoa yote na kazi yao KUU ni "KUNYOOSHA MIKONO' cha ajabu ni wazima wa afya!

    ReplyDelete

  6. Ombaomba walishajaribu sana kusaidiwa na Serikali kwa kurudishwa kwenye "vijiji vya ujamaa".
    Wanapewa ARDHI msaada gani zaidi ya hapo mtu unapata?
    HUYU MZEE KAMA ANAVYOSEMA MWENYEWE KAANGUSHWA NA WATU WAKE WA KARIBU WALIOFUJA "MALI" ZAKE, SIO SERIKALI.
    MAANA ALISHAOMBA AKAPATA MTAJI WA KUTOSHA KAMA MWANAWE ANAVYOTOA USHAHIDI.

    KIFO CHA MATONYA ISIWE SABABU YA KULAUMU SERIKALI.
    ALIOMBA AKAPATA. AKASHINDWA KU "MANAGE"

    HE CHOSE TO BE A BEGGAR FOR LIFE.

    ReplyDelete
  7. RIP Matonya. Namkumbuka sana mwaka 1984 alikuwa anaomba Posta Mpya na kariakoo hap Dar es salaam kabla ya kupewa transfer na Makamba na kumpeleka Morogoro. Style yake ni hiyo hiyo ya kulala chini. Inasikitisha sana kwa kweli, alikuwa mlemavu wa macho! Wengi wanaomba kwa kukosa msaada, na hizo kambi za maskini na wazee zina khali mbaya sana, ndio maana hutoroka na kwenda kuomba. Ni dona na maharage tangu asubuhi mpaka usiku. Mbuzi na pilau ni kipindi cha Eid na Christmas tu. Watanzania tuwe na mazoea ya kuwasaidia wenzetu wenye matatizo!

    ReplyDelete
  8. Mwenyezi Mungu ampumzishe Mzee wetu, ambaye aliwakilisha taswira ya nchi, ni kweli ni msiba wa Taifa.

    Mnaokataa hapo juu, au kujiuliza kwa nini ombaomba hawaishi hapa mjini mnatakiwa mjiulize swali kubwa zaidi: kwa nini Tanzania kama taifa tumekuwa ombaomba miaka yote hii?? Tumepewa hizo pesa kwa nini hazijatusaidia??

    Na tuazimie sasa, kwamba kifo cha huyu Mzee (taswira ya taifa) huwe ndio mwisho wa sisi kuwa ombaomba, maana tumetumia stahili nyingi za kuomba lakini hamna kitu. Twende kazini!!

    Mungu awabariki watu wote!!

    ReplyDelete
  9. Kwa baadhi ya makabila OMBAOMBA ni HOBBY. Matonya alikuwa akifukuzwa ili apate msaada wa bure na alikuwa akipata hifadhi Fungafunga akawa anatoroka. Na amefukuzwa sana asiiombe ila ni hobby. Tusione picha ya ombaomba tukalaumu serikali bila kujua.

    Kumbuka pia hao watu ni matajiri sana. They make a lot of money kwa kuomba. Usiku wanapiga ulabu kuliko mimi nawewe. Its a culture na sio serikali. Especially kwa Matonya amepata umaarufu kwa kufukuzwafukuzwa na anarudi.

    ReplyDelete
  10. If all other things remain constant naweza sema Maisha tunayoishi ni uchaguzi wetu wenyewe japokuwa kwa miaka hii wakati mwingine mambo kama ufisadi na kupendeleana yameharibu nyota ya baadhi ya watu, kuilaumu serikali kwamba imeshindwa kumwezesha matonya kama alivyochangia mdau wa kwanza tunakuwa hatuitendei haki kwani Matonya ni mtu mzima na ameanza kuomba tangu miaka mingi iliyopita kama mdau mmoja aliechangia kumwona matonya posta na k/koo since 1984 ambako pamoja na hali ngumu ya kiuchumi lakini mfumo uliokuwepo enzi hizo ulimwezesha mtu kuishi japo kibishibishi kwani mafisadi walikuwa hawana nafasi kama sasa na alikuwa na nguvu zake. KUDAI KWAMBA SIJUI NI MZEE NAPO SI KWELI HUYU AMEANZA KUOMBA TANGU KIJANA HIVYO NI TABIA YAKE HATUWEZI KULAUMU SERIKALI HAPA LABDA KAMA ANGEKUWA AMEANZA KAZI HII UKUBWANI TUNGESEMA MFUMO ULIOPO UMEPELEKEA KUWA HIVYO

    ReplyDelete

  11. "Matonya alikuwa taswira ya Taifa" WRONG!!

    Tanzania yetu ni TAJIRI
    Matonya alichagua kuwa masikini na ombaomba.
    Alipata "akasusa" kuwa na 'mali' akaamua awe ombaomba for life which he did.

    TZ S I O MASIKINI, ILA NI TABIA YA KUOMBA NDIYO ILIYOJENGEKA TOKA AWAMU YA KWANZA.

    ReplyDelete

  12. Kiongozi wa awamu ya kwanza aliwahi kuitwa professional beggar.

    ReplyDelete
  13. RIP MZEE! Yeye na Mkuu tofauti yao ni maeneo ya kuomba tu!

    ReplyDelete
  14. Wewe anon wa Aug 26, 08:44 AM.

    Mkuu uliyemkusidia wala SIYE!!

    Mkuu wa kuomba mpaka akapachikwa jina la ombaomba alishavuta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...