Sehemu ya kuingilia abiria likikarabatiwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza
 Sehemu ya abiria ndani ya jengo hilo lina viyoyozi vinavyomwaga maji na kutoa raha abiria
Vigari vya kubebea mizigo ya abiria
 Mkusanya ushuru wa magari akipitia madereva kuchukua pesa kabla ya kufungua 'geti' kuruhusu magari yatoke nje ya uwanja. 
 Mtindo wa uwanja wa ndege wa Mwanza kwa madereva siku hizi ni kuingia bure, kutoka pesa...
Geti linaendeshwa kwa nguvu ya binadamu, na mvua na jua ni dhahiri mfanyakazi anapambana navyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Shame!! Shame!! Shame!!!
    Mkoa wenye dhahabu na sangara wa export ndio una uwanja wa ndege namna hii miaka yoote hii.. haiingii kabisa akilini kama kweli tuna viongozi Tanzania....
    Mimi

    ReplyDelete
  2. Afadhali kwa kweli....binafsi nilikuwa sijawahi kuona uwanja mchafu kama wa Mwanza..lol yani kama stendi ya Ubungo vile..mbu, nzi nahisi hata kunguni walikuwepo....aibu tupu...nikawa najiuliza hivi hawa viongozi wanafikiri nini haswa? na wanapita hapo kila siku...uchakavu sio sababu ya kutunza uchafu jamani watanzania tubadilike.....can u imagine hiyo sehemu ya kusubiria kuondoka 'departing lounge ilikuwa haina hata dustbin.....aliyekula mayai, maembe biscuit soda za kopo toka asubuhi anaacha uchafu wako kwenye kiti au chini na hamna wa kusafisha...lol nilikuwa na wageni siku hiyo sijawahi kuaibika kama hivyo

    ReplyDelete
  3. Wote mlionena hapo juu mmesema ukweli, mimi nimepita Mwanza many times. Tusiseme haibu, bali UZEMBE UZEMBE UZEMBE.. Minofu ya samaki, madini, pamba, vyote ni international commodities na bado tumeshindwa kujenga uwanja wa maana. Ukiwa 7ft huwezi simama ndani ya departing lounge ya Mwanza.

    Nilipita na mjerumani anatoka Arusha, akaniuliza 'I thought Mwanza one of the biggest cities in Tanzania'? Nikasema YES. Akasema did the pilot land at the wrong airport? kwa haibu nikasema NO...

    ReplyDelete
  4. Maganda ya ndizi, chupa za maji na maganda ya biskuti nalo ni kosa la Mwakyembe? Mnadhani dhahabu ndiyo zinazoleta ustaarabu? Timiza wajibu wako!

    ReplyDelete
  5. Dr. patrick nhifulaFebruary 03, 2013

    michuzi,
    Magazeti nhigula anasema unajuwa mfumo wetu wa utawala siyo mbaya bali ni watu wasivyo kuwa wakweli na uwazi juu ya watawala na viongozi wao juu ya kutoweza kutambuwa nini hasa ni matatizo. serikali watasema hawa fedha za kuendesha uwaja wa ndege. Mbona watu wa mwaza wasijenge hoja ya kuendesha uwanja wa mwaza ka ma biashara ya serikali na watu binafsi? Mimi binafsi ninaona lazima wananchi wawe mbele na kujenga hoja binafsi badala ya ya kusubiri serikali

    ReplyDelete
  6. acheni uswahili, they will clean it when JK and/or Dr Mwakyembe are passing thru

    ReplyDelete
  7. Ndio maana wana Mtwara wameanza kufumbua macho yao mapema. Mali inayotoka kwenye sehemu kwanza iendeleze sehemu hio. na pia viongozi wawajibishwe na wananchi wa sehemu hiyo. Kwa upande wa usafi,haitaki bajeti kubwa isipokua huu in UZEMBE wa mkuu wa airport na kwa tabia hii alionayo hafai kabisa kuwa kiongozi.

    ReplyDelete
  8. Mwanza jengo la airport kw aujumla ni Uzmbe usioweza elezeka, kuna trip ngapi za ndege to mwanza? nyongi sana tu. Why jengo pawe na jengo kama stand ya mabasi ubngo? check in, arival mess , mes mess everything, ukifika usiku ukakuta wale wadudu kama kumbikumbi ndo utachoka na huo uwanja, waiting lunge hali ya hewa taabu, kuchafuuuu, all those years kwanini mambo yasirekebishwee? kamata migodi yote iweke hela hapo sio kukimbizia ulaya na south africa.
    Mi mchagga lakini wenzangu wasukuma amkeni kwa hili jamani khaa inatisha pale.

    ReplyDelete
  9. Sasa pamoja na mwonekano mbovu na matengenezo yanayofanywa hapo uliza gharama ni kiasi gani zimetoka?

    Loooo utaandikiwa tarakimu yenye MASIFURI KIBAO YANAFOFUATIA, kuashiria ya kuwa gharama iliyotumika ni kubwa mno!

    ReplyDelete
  10. Umfikia wakati sasa, tuendeshe uchumi wa Kimikoa na kuunganisha kwenye Uchumi mkuu wa nchi.

    Ni kama tunavyoona mchango mkubwa wa Mkoa wa Mwanza katika kujenga uchumi wa Tanzania kwa idadi kubwa ya rasilimali zinatotokea hapo tunaona kabisa havilingani na maendeleo yanayo onekana hata kwa macho hapo Mwanza.

    Hebu fikiria tokea Uhuru mwaka 1961 sasa ni miaka zaidi ya 51 mali zinavunwa Mwanza,

    MALI:

    -ALMASI,
    -DHAHABU,
    -PAMBA NA MAZAO YAKE,
    -NG'OMBE NA MAZAO YAKE,
    -SAMAKI,
    -BIDHAA ZA MALI ASILI,
    -MADINI MENGINEYO.

    Halafu tunakuja kuona Zanzibar wanalalamika ya kuwa wananyonywa, mbona Mwanza hawakulalamika kwa Alamasi na Dhahabu yao wakati inajulikana sana ya kuwa Maduka yote ya Masonara wa Vito vya Dahahabu Zenji wanapata malighafi ya dhahabu kutoka Mwanza?

    Umefika mwisho sasa tuseme TANZANIA BILA WIZI INAWEZEKANA!

    ReplyDelete
  11. wakuu hii ni kweli ni uwanja wa ndege au utani mpaka saa hii sijahamini kabisa mimi nilijua jamaa wanafanya marekebisho ya baa zetu za uswahilini kweli mungu tusaidie tanzania

    ReplyDelete
  12. Haaaa,,,hivi ninaota au ni kweli?

    Ukisikia Bongo Tambarale ni kama hapa Mdau Anony wa Mon Feb 04, 12:23:00 pm 2013

    Huo ni Uwanja wa Ndege Mwanawane, mahala ambapo hata Obama akija atake kwenda Mwanza atatua hapo na ndege!

    Bongo ndio kama tuijuavyo!

    ReplyDelete
  13. Nafikiri Ankali Michuzi kutokana na safari aliyorudi na uchovu alionao amekosea kurusha Taarifa!!!,

    Mwanawane, safari kutkea Davosi-Swiss aliyopiga Mjomba Michuzi mchezo?, unalala kwenye ndege unazinduka unambiwa ndio kwanza mpo Misri!

    LABDA PICHA HALISI YA UWANJA WA NDEGE MWANZA ANKALI AMEIPOTEZA AU IMEFUTIKA KWA BAHATI MBAYA KWENYE MTANDAO, WAKATI ALITUMIWA TAARIFA ZA KUKAMILIKA HATUA ZA MWISHO ZA UJENZI WA BAA MOJA KULE TANDALE KWA MTOGOLE KWA WANA YANGA S.C PAMOJA NA PICHA YAKE!

    ''Hivyo hilo Banda kubwa hapo ni Baa moja huko Tandale kwa Mtogole, inamaliziwa kujengwa'' NA SIO SEHEMU YA MAPUMZIKO YA ABIRIA KTK UWANJA WA NDEGE MWANZA!

    MMENIPATA HAPO?

    ReplyDelete
  14. Mwonekano mbovu wa Uwanja wa Ndege Mwanza, hiyo ndiyo gharama halisi ya kuubeba Ufisadi!

    ReplyDelete
  15. Picha ya chini Geti:

    Hiyo kazi ya Geti linaloendeshwa kwanguvu ya binaadam inatakiwa muhusika ajiandae kwa mambo haya:

    1.Ale dona la uhakika, maana shusha mapndisha ya hilo chuma atapoteza nishati nyingi mwilini!

    2.Awe na koti la mvua kama itatokea!

    3.Awe na singileti kwa wakati jua likiwa kali inahitaji avue makotimakoti na mibuti abaki na singileti!

    ReplyDelete
  16. Leo afadhali nimepata nafasi ya kusema dukuduku langu uwanja wa ndege Mwanza. Ukiwasili mnaenda kusimama kusubiri mizigo yenu ishushwe, mizigo inapoletwa hakuna utaratibu wa kuchukua ni kupigana vikumbo tu, hii sio ustarabu nafikiri wafanyakazi wa uwanja huu wanatakiwa kuwa wabunifu kutatua tatizo hili. Nawashauri kwamba badala ya kuitupa na watu kugombania mizigo yao waipange mstari chini ya kile kibaraza watu wapite kwa mstari watambue mizigo yao. Kinachofanyika pale ni kero kubwa. Badilikeni. Mdau wa MIchuzi Blog.

    ReplyDelete
  17. NYIE WOTE HAMJAONA MAAJABU AMBAYO MIMI NIMEONA KWENYE UWANJA WA NDEGE MWANZA,NADHANI NCHI NZIMA HAKUNA UWANJA MCHAFU KAMA HUU,SEHEMU YA KUKAA CHINI YA VITI KULIKUWA NA MAVI MENGI NA JUU YA MAVI KULIKUWA NA MAGANDA YA NDIZI NA MAGANDA YA MACHUNGWA,WAKATI WA MVUA PANAVUJA WANAWEKA NDOO KATIKATI MAJI YADONDEKE HUKO.HUYU KIONGOZI WA MWANZA SIJUI KAZI YAKE NINI?MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  18. Suala ni kuwa tunaviongozi ambao wana mawazo bado ya enzi za ujamaa ambao umekwisha shindwa. Hata kama mkilaumu CCM bado haitasaidia suala ni kubadilika jinsi ya kufikiria na kufanya mambo ndani ya Tanzania. Mimi binafsi ni Mtanzania lakini nimechoshwa na Watanzania jinsi mlivyokuwa wavivu wa kufikiria kila siku kulaumu serikali bila ya kutoa mapendekezo jaribuni kuwa watu wa kuwa na mawazo endelevu. Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe sio wawekezaji suala ni kuangalia jinsi gani wawekezaji waatasaidia kusuma gurudumu la maendeleo na sio kuwaona kama ndio wakombozi bali ni mapartner wetu tufanye nao kazi pamoja kwani nao wametumwa na mashareholder wao kuja kutengeneza faida sio kukusaidia wewe Mtanzania maana kila mwaka lazima wawalipe gaiwo mashareholder wao kwahiyo narudia kusema kuwa Tanzania nzuri itajengwa na Watanzania wenyewe sio zaidi ya hapo na wala sio CCM wala chadema wala CUF hivi ni vyama tuviambie ni sera zipi zitafanyikisha maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na baadae hayo maendeleo yataleta maendeleo ya Taifa na vizuri ni kwa vyama vya siasa au chama kilicho madarakani kuhubiri sera na kuelimisha Watanzania kuwa sera hizi ninakuwezesha kuendelea na wajibu wako kama Mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kunufaika na hizi sera na sio kusubiri serikali ikufanyie kila kitu hakuna serikali duniani ambayo inaweza kukupa utajiri wabure bila kufanya kazi. fanyeni kazi kwa bidii Wanzania hili tuweze kupata maendeleo.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  19. Kwa kuwa wadau wengi wanaonekana kuwa na uchungu na wizi nadhani imefika wakati sasa wa kuwa na mfumo unaruhusu kufuatilia vyanzo vya mapato ya watu bila kujali anafanya kazi serikalini au ili kupata uwiano wa mali na mapato maana hao waizi wananjia nyingi za kujificha!


    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...